Na VENANCE JOHN
Mgombea urais wa chama cha Republican Donald Trump jjana alionya kwamba, ikiwa atachaguliwa, ataiadhibu Mexico na China kwa ushuru isipokuwa nchi zote mbili zitaamua kusimamisha kuingiza madawa aina ya fentanyl nchini Marekani.

Katika mkutano wa kampeni huko Pittsburgh, Pennsylvania, Trump alisema atachukua hatua haraka kukabiliana na ulanguzi wa dawa za kulevya kwenye mpaka wa Kusini wa Amerika na Mexico.
"Tutasimamisha mara moja dawa hizo kumiminika katika mpaka wetu," alisema Trump. Trump alisema atatoza ushuru kwa bidhaa kutoka Mexico kwa 25% na atafanya kitu sawa na hicho kwa China kwani nchi hiyo inasafirisha dawa za fentanyl kwenda Mexico.
"Kila kitu wanachouza Marekani kitakuwa na ushuru wa asilimia 25 hadi watakapoacha kuingiza madawa za kulevya. Na niwaambie kitu, dawa hizo zitakoma haraka sana hata kichwa chako kitazunguka. " Trump alisema.
Trump, katika mkutano wake wa hadhara, pia aliendelea kusisitiza kuwa atawafukuza kwa wingi wahamiaji wanaoingia Marekani iwapo atachaguliwa katika uchaguzi ambao unafanyika leo.
Comments