top of page

MAREKANI USO KWA USO NA URUSI LEO

Na VENANCE JOHN


Vyombo kadhaa vya habari nchini Marekani na Urusi vinaripoti kuwa mazungumzo ya kumaliza vita vya Ukraine yanatarajiwa kuanza leo Jumanne katika mji mkuu wa Saudi Arabia, Riyadh. Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Marco Rubio, Balozi wa Marekani katika Mashariki ya Kati, Steve Witkoff, na Mshauri wa Usalama wa Taifa, Mike Waltz, wote wamesafiri kuelekea katika nchi hiyo ya Ghuba kwa ajili ya mazungumzo ya awali.


Kwa upande wa Urusi, Waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Sergei Lavrov, pamoja na mshauri wa Rais Vladimir Putin, Yuriy Ushakov wanatarajiwa kushiriki katika mazungumzo hayo, kwa mujibu wa vyombo vya habari vya serikali ya Urusi.


Watendaji hao wanawawakilisha Trump na Putin, kufuatia mazungumzo ya awali kwa njia ya simu kati ya viongozi hao yaliyofanyika wiki iliyopita. Hata hivyo Ukraine haijaalikwa kushiriki katika mazungumzo haya yanayofanyika Riyadh, jambo ambalo limezua wasiwasi miongoni mwa viongozi wa Ulaya.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page