Na VENANCE JOHN
Marekani imesitisha zaidi ya dola milioni 13 za ufadhili unaotolewa na nchi hiyo kwa operesheni ya vikosi vya usalama vya kimataifa vinavyopambana na magenge ya uhalifu nchini Haiti. Umoja wa Mataifa umesema ufadhili huo umesitishwa kwa muda wa siku 90.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_3a3b442322e64bd599369a3a429a8007~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_3a3b442322e64bd599369a3a429a8007~mv2.jpeg)
Haya yanajiri baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kuagiza misaada ya nje ya Marekani isitishwe, ili ihakikiwe na kusukwa upya kuendana na maslahi ya taifa lake. Magenge hatari ya uhalifu yaliyo na silaha zinazodaiwa zimetoka Marekani wapo katika mji mku wa Port-or- Prince wakidhibiti mji na kuvamia maeneo tofauti nchini Haiti.
Misheni ya usalama ya kimataifa iliyoidhinishwa na baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, sio operesheni ya Umoja wa Mataifa bali inategemea misaada kutoka mataifa yaliyoendelea. Katika misheni hiyo kufikia sasa kuna zaidi ya maafisa wa polisi 900 kutoka Kenya, vikosi vya El Salvador, Jamaica, Guatemala na Belize.
Zaidi ya dola za kimarekani milioni 110 zimewekezwa katika mfuko wa misheni ya UN, kiasi kikubwa kikitoka Canada, kulingana na data za Umoja wa Mataifa. "Marekani iliahidi kutoa dola milioni 15 kwa mfuko huo wa kufadhili operesheni hiyo, dola milioni 1.7 zilikuwa tayari zimetolewa.
Comments