top of page

MAREKANI YAPANGA KUITENGANISHA GOOGLE, CHROME, ANDROID NA GOOGLE PLAY, YAISHUTUMU KWA UKIRITIMBA WA MTANDAO

Na VENANCE JOHN


Idara ya haki ya marekani imeitaka program ya kuvinjari katika mtandao wa intaneti ya Google kutenganishwa na kivinjari cha chrome, program endeshi ya simu ya Android, na hifadhi ya program tumizi nyngine (play store)kwa kile idara hiyo inachosema kwamba Google anazuia makampuni mengine kukua.


Google mara kadhaa amekuwa akishutumiwa kwa kufanya njama ya kuua ushindani kutoka kwa washindani wake kama DuckDuckGo, Bing miongoni mwa wengineo wengi.


Idara ya haki ya Marekani (DOJ) imesema inaweza kumtaka jaji kuilazimisha Google kuacha sehemu za biashara yake kama vile kivinjari chake cha Chrome na mfumo wa uendeshaji wa Android, kwani kampuni hiyo imekuwa ikidumisha ukiritimba haramu katika mfumo wa utafutaji mtandaoni.


Google imekuwa ikilalamikiwa kwa kukusanya data nyeti za watumiaji, na kutomruhusu mtumiaji kupata maudhui anayotafuta kwenye vivinjari vingine.


Karibu simu zote zinazotumia mfumo endeshi wa Andoid, huja na kivinjari mama (default App) cha Google na Chrome kitua ambacho kinamnyima uhuru mtumiaji wa simu kufanya uchaguzi wa aina ya kivinjari anachohitaji. Google ambayo imechukua himaya katika mtandao ikiwa itagawanywa, hatua hiyo inaweza kupunguza mapato yake huku ikiwapa wapinzani wake nafasi zaidi ya kukua.


Tabia ya Google ya ukiritimba imedhoofisha watoa huduma wengine wa huduma za utafutaji mtandaoni ( browsing) na uwezo wa wasindani wake kuchuma mapato ya matangazo . Hatua hiyo imeelezwa na idara ya haki ya Marekani (DOJ) kama kuiruhusu Google kunufaika kutokana na matangazo ya maandishi huku ikiwakandamiza washindani wake.

Comentarios


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page