top of page

MAREKANI YASITISHA USHURU BAADA YA COLOMBIA KUKUBALI NDEGE KUWARUDISHA WAHAMJIAJI

Na VENANCE JOHN


Marekani imesema haitaendelea na ushuru wa forodha kwa Colombia, baada ya nchi hiyo kukubali kupokea bila vikwazo wahamiaji waliofukuzwa na utawala wa Donald Trump. Donald Trump alikuwa ameamuru ushuru wa 25% kwa bidhaa zote za Colombia baada ya rais wa Colombia, Gustavo Petro kuzuia safari mbili za ndege za jeshi za Marekani kutua nchini humo siku ya jana Jumapili.


Rais wa Colombia Gustavo Petro awali alijibu kwa kusema kuwa nchi yake itawapokea raia waliorudishwa makwao kwa ndege za kiraia, bila kuwachukulia kama wahalifu. Taarifa ya ikulu ya Marekani White House inasema Colombia sasa imekubali kuwapokea wahamiaji wanaowasili kwa ndege za kijeshi za Marekani bila kikomo au kuchelewa. Colombia ilisema mazungumzo yatadumishwa ili kuhakikisha utu wa raia wao.


Rais Petro awali alikataa kuingia katika ndege za kijeshi za Marekani za kuwafukuza, akisema kwamba wahamiaji wanapaswa kurejeshwa kwa heshima huku naye alikuwa ametangaza kuwa hata yeye ataweka kodiya 25% kwa bidihaa za Marekani. Kujibu, Trump alitangaza hatua za haraka na za kulipiza kisasi katika chapisho kwenye mtandao wake wa kijamii wa Truth Social, ikijumuisha ushuru na vikwazo vya visa.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page