Na VENANCE JOHN
Ikiwa kwa sasa mwanamuziki wa Marekani Sean Diddy Combs maarufu kama Diddy ambaye kwa anashikiliwa kwa tuhuma za unyanyasaji wa kingono wiki iliyopita imeripotiwa kuwa mauzo ya nyimbo zake yamepanda na kupata ongezeko kubwa la wasikilizaji katika kazi zake kupitia mitandao ya kuuzia muziki.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_af013742623f4a4c8ac83576c24185f5~mv2.jpg/v1/fill/w_526,h_526,al_c,q_80,enc_avif,quality_auto/57c8da_af013742623f4a4c8ac83576c24185f5~mv2.jpg)
Tovuti ya ABC News, imeeleza kwamba kampuni ya Luminate, inayoshughulika na takwimu za muziki imeripoti kuwa muziki wa Diddy ulipata ongezeko la wasikilizaji asilimia 18.3 kwa wiki iliyoisha.
Hata hivyo sio jambo la kushangaza kupanda kwa kiwango cha kusikiliza muziki wa msanii inapotokea msanii kukutana na tuhuma fulani, kwani mwanamuziki R.Kelly baada ya kutuhumiwa kwa unyanyasaji wa kingono kwa wanawake na wasichana wadogo idadi ya usikilizaji wa nyimbo zake iliongezeka mara dufu zaidi ya awali.
Ukiachilia mbali ongezeko hilo inasemekana huenda Diddy alihisi ipo siku atakamatwa kutokana na sherehe alizokuwa akifanya nyumbani kwake. Hiyo ni kutokana na moja ya mahojiano yake aliyofanya mwaka 1999 alisikika akieleza kuwa ipo siku Polisi watamkamata.
Msanii Diddy hata hivyo ni kama alikuwa anafahamu kuwa siku moja atakuwa matatani kwani kwenye mahojiano mwaka 1999 alikunukuliwa akisema kwamba siku moja atakamatwa na sherehe zake zitafungwa.
“Mtakuja kusikia kuhusu sherehe zangu, watazifunga. Huenda wakaanza kunikamata, kufuatia na mambo yote ya ajabu tunayoyafanya kwenye sherehe zangu. “Lakini mimi nafanya sherehe kwa ajili ya kufurahi na kuleta watu pamoja kutoka sehemu zote za maisha,” alisema Diddy kwenye mahojiano yake na Entertainment Tonight
Diddy alikamatwa Jumatatu Septemba 16, na kupelekwa katika gereza la ‘The Metropolitan Detention Center (MDC)’ kwa tuhuma za ulaghai wa kingono na usafirishaji wa binadamu ili kujihusisha na biashara ya ngono na ataendelea kusota mahabusu baada ya kukataliwa dhamana.
Comments