top of page

MAYELE AELEZA ALIVYONUSURIKA KUKATWA MGUU WAKATI ANAENDA KUSAINI PYRAMIDS, HADI NIKAOMBEWA NA MWAMPOSA..




Aliyekuwa mshambuliaji wa Yanga Fiston Mayele anayekipiga Pyramids ya Misri kwa sasa amefanya mahojiano kwenye kipindi cha Wednesday Night Azam TV ambapo ameeleza kuwa alipitia hali ngumu sana Kimwili na Kisaikolojia, kwani kabla ya kwenda kusaini mkataba katika klabu ya Pyramids ya Misri Mguu wake ulianza kuvimba na kumuuma sana.

Akawa anatembelea magongo, analala sebuleni kwani alikuwa hawezi kupanda ngazi za chumbani kwake, anaongeshwa na kufanyiwa kila kitu na mkewe, na mguu ulikuwa hatarini kukatwa kama ungeoza, hali hii ilimfanya kuona kuwa hataweza kucheza mpira tena katika maisha yake akawa akawa analia usiku na mchana.

Muda huo Pryamids walikuwa wakimuita aende kusaini mkataba hali iliyomfanya kuwadanganya kuwa amefiwa ili avute muda hadi apate nafuu, ikambidi aende kwao Congo ndipo akapata nafuu akaenda kusaini mkataba na siku tatu mbele Pyramids walipo-post picha yake kwenye mtandao wao ya kijamii, mguu ukavimba tena na kuanza kumuuma mno.

Akarudi Tanzania na kwenda kuombewa kwa Mchungaji Mwamposa na akapata nafuu, na sasa anacheza hivohivo huku mguu ukiwa umevimba lakini kwa sasa hauna maumivu.

"Baada ya ile mechi ya dodoma nililia sana niliumia mguu ulivimba hata kutembea sikuweza, hospitali walisema nimevunjika lakini hawawezi kuniweka hogo maana mguu umevimba utaoza alafu watanikata hivyo natakiwa nikae tuu hadi mguu upungue, nikaanza kuwaza vitu vingi nikasafiri kwenda Congo.

"Nilivyoenda Congo Mungu akasaidia nikawa sawa nikaenda Pyramids kusaini walivyonitambulisha kesho yake nikaamka mguu umevimba tena nikasema hapana, nikarudi tena Congo Kisha Tanzania nikaenda kwa Mwamposa akanisaidia mguu ukarudi kidogo.

"Mpaka Leo mguu wangu mmoja umevimba haujarudi kama zamani, hakuna maumivu Lakini mguu mmoja ni mkubwa kuliko mwingine," Mayele.

Mayele ameongea yote haya huku akisisitiza kuwa mwisho wa msimu huu ataongea kila kitu.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page