top of page

"MAZURI YANAKUJA JANGWANI" ALLY KAMWE

Kutoka kwa Meneja habari na mawasiliano Yanga SC Ally Kamwe amefunguka haya

"Alhamdulillah, Kwenye upande wa Football, kwa hii misimu miwili Uongozi wetu chini ya Rais @caamil_88 umefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana

Mara 2 Champions wa Ligi [Msimu huu In shaa Allah wanasaka la 3]

Mara 2 Kombe la Azam Sports Federation




Mara 2 Ngao ya Jamii

Medali ya Mshindi wa pili Caf Confederation Cup

49 Records ya Unbeaten kwenye Ligi

Tayari Tuna Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa

Ziko rekodi nyingi zaidi Klabu yetu ya @yangasc imeziweka kwenye Pitch chini ya Uongozi wetu huu wa sasa hivi, Tena ni katika kifupi mno.

Wakati Tukiendelea kufurahi na Ubora wa Timu yetu uwanjani, Uongozi wetu haujabweteka na kutumia mafanikio hayo kama kichaka cha kutokufanya Maendeleo mengine ya Klabu yetu.

Yako mambo Mawili muhimu mbele ambayo Yanatakiwa kufanyika kwa sasa.

1: Hatua ya pili ya Mchakato wa Mabadiliko

2: Ujenzi wa Uwanja wa Yanga

Wengi wamekuwa wakijiuliza kuhusu nini kinafata baada ya Phase ya kwanza ya Transformation kukamilika.. Lakini ni Lini @yangasc Uwanja wetu Utakamilika

Maswali haya Mawili, hivi karibuni Yatapata majibu yake.. Majibu Yatakayotupa Furaha zaidi Wananchi na kuendelea kujivunia kuchagua kushabikia @yangasc Yetu, Jambo zuri kwetu, Hamna atakayeuzwa wala kukopwa. Tukae Tayari Wananchi... Kikao Maalum cha Kamati ya Utendaji kimekaa Leo kwa ajili ya Ajenda hizo kubwa 2 zenye manufaa makubwa na Klabu yetu Mazuri yanakuja Jangwani." Amefunguka Kamwe.

Comentarios


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page