top of page

MBEBA VYUMA MICHAEL CHIDOZIE AFARIKI WIKI KADHAA BAADA YA KUPIGWA RISASI NA MKEWE KWENYE UGOMVI...

Mbeba vyuma mwenye asili ya Nigeria anayeishi Marekani, Michael Chidozie amefariki chini ya mwezi mmoja baada ya polisi kusema kuwa mkewe alimpiga risasi mara nyingi nyumbani kwao huko Houston, Texas, Marekani.


Ilifahamika kuwa Chidozie alifariki baada ya kupigwa risasi mara kadhaa na mkewe, Keaiirra Shavoiyae Chidozie kutokana na ugomvi kati ya wanandoa hao mnamo Machi 21.

Mail Online inaripoti kwamba Michael, 26 alipigwa risasi na mkewe katikati ya mabishano mbele ya watoto wao nyumbani kwao huko Houston mnamo Machi 21.

Wakati wa mabishano hayo, mkewe alitoa bunduki na kumpiga risasi mme wake mara kadhaa.

Alikimbizwa katika Hospitali ya Ben Taub baada ya polisi kumpata akiwa na majeraha ya risasi huku mkewe akiwa katika hali ya hofu katika eneo la maegesho lililo karibu na nyumbani kwao akiwa amewashikilia watoto wao wawili, wenye umri kati ya miaka mitatu na miwili.

Polisi walimshikilia mke wake na kumfungulia mashtaka ya kumpiga risasi huku watoto wakitunzwa na moja ya wanafamilia. Haikuwa rahisi kwa upande wake Chidozie aliekuwa hoi kwa kutafuta msaada wa maisha yake lakini jeraha baya la uti wa mgongo lilipelekea kufariki kwake baada ya maumivu yaliyodumu kwa siku 18 tangu kupigwa risasi.

Alidai kumpiga risasi Chidozie ili kujilinda huku akihofia maisha yake wakati wa ugomvi alipomfuata chumbani kwao.

Haijulikani mabishano hayo yalisababishwa na nini, Wakati huo huo, Keaiirra, 28, ameachiliwa kwa dhamana na anatarajiwa kufikishwa mahakamani tena Mei 23.

Usiache kufuatilia Msasa Online kwa habari zaidi tembelea tovuti yetu www.msasamedia.com

Komentáře


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page