top of page

MBOSSO APONA UGONJWA WA MOYO

Anaandika Mbosso


"Mnamo tarehe 28 mwezi wa 12 mwaka 2024 nilipata nafasi Ya kushiriki kwenye zoezi la upimaji wa Afya Ya Moyo lililofanyika katika Taasisi Ya Moyo Jakaya kikwete (JKCI) Kawe Jijini Dar Es Salaam Zoezi hili liliandaliwa na Mheshimiwa Rais @samia_suluhu_hassan kwa ushirikiano wa Taasisi ya JKCI na @basata.tanzania na @tanzania_film_board ikilenga kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu kufuatilia hali ya afya ya moyo na kuzuia magonjwa yanayoweza kuzuilika


Kupitia zoezi hili iligundulika ninashida ya Moyo ambayo nilizaliwa nayo kitaalamu niliambiwa ni shida ya Umeme wa Moyo ambayo Taasisi ya JKCI wakishirikiana na Basata waliahidi kunisaidia na kupona kabisa


Alhamdulillah. Siku Ya juzi kuja Jana ilikuwa na masaa 12 hadi Kutimia 24 yenye hofu kubwa kwangu ambayo yameleta matoke Ya furaha na amani ya milele kwangu, Familia yangu na kwa Mashabiki wote wa Mziki Wangu


Nilipata nafasi yakutibiwa na Madaktari bingwa kabisa wa Maswala Ya moyo kutokea Misri (Egypt) sambamba na Madaktari kutoka nyumbani hapa hapa Tanzania ndani ya Lisaa Moja Tu na kila kitu kukamilika


Kwa sasa Kijana Wenu nimepona kabisa ugonjwa wa moyo uliokuwa unanisumbua kwa kipindi cha miaka yote na Jana jioni nimeruhusiwa kuendelea na mapumziko nyumbani na baada Ya Wiki 1 niweze kuendelea na majukumu yangu ya kila siku.


Shukrani zangu nyingi za dhati zikufikie Popote Ulipo Mheshimiwa Rais wetu Tanzania Mama Yangu @samia_suluhu_hassan Asante sana Mama chini ya Utawala wako yanawezekana ambayo niliaminishwa hayatawezekana hadi niende India.. Asante Sana Mama Kijana wako Sasa ni Mwenye Afya iliyo ngangari na nakuahidi nitashikamana na wewe Mkoa kwa Wilaya, Vijiji kwa vitongoji kuhakikisha natangaza sifa za utendaji wako wa Kazi


Asante sana katibu mtendaji wa Basata @kmapana kwa mchango wako mkubwa kwenye kufanikisha hili. Shukrani zangu zikufikie Mkurugenzi Mkuu JKCI Dokta . PETER KISENGE kwakuwa na mimi Bega kwa Bega kuhakikisha natibiwa vizuri na napona Kabisa wewe sambamba na Madaktari na Wauguzi wote wa JKCI Muhimbili mlifanya hospital nipaone tu kama nipo nyumbani. Asante Sana Mashabiki Zangu Wote Kwa Dua Zenu. Sasa nimepona na kazi iendelee".

Commentaires


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page