top of page

MBOWE AMPONGEZA LISSU KWAUSHINDI, AMTAKIA KILA LA KHERI

Baada yaTundu Lissu kumuondoa Freeman Mbowe kwenye kiti cha Uwenyekiti wa Chadema kwenye uchaguzi uliofanyika usiku wa kuamkia leo. Tundu Lissu ameshinda kwa kishindo nafasi ya Uwenyekiti wa Chadema dhidi ya mpinzani wake mkubwa Freeman Mbowe ambaye amehudumu nafasi hiyo kwa miaka zaidi ya ishirini.


Wawili hao walichuana vikali katika kinyang'anyiro hicho kila mmoja akionyesha umwamba wake hali ambayo ilisababisha uchaguzi kuwa na msisimko mkubwa. Sasa Mbowe kupitia ukurasa wake wa X zamani Twitter ametoa pongezi hizi kwa Lissu


"Nimepokea kwa mikono miwili maamuzi ya uchaguzi wa Mkutano Mkuu wa Chama chetu CHADEMA uliohitimishwa leo asubuhi 22 Januari 2025. Nampongeza Mhe. Tundu Lissu nawenzake kwa kuaminiwa kutwikwa jukumu la Uongozi wa Chama. Nawatakia kila la kheri katika kukipeleka mbele Chama chetu."

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page