top of page
Radio on air

MBUNGE SANTIEL KIRUMBA ASHAURI KILA LINE YA SIMU IKATWE TSH 5O KWA AJILI YA UJENZI WA BARABARA....

Kutoka Bungeni Dodoma Mbunge wa Viti Maalum Santiel Eric Kirumba ameishauri Serikali kuweka makato ya Tsh. 50 kwa kila laini ya simu kwa ajili ya Mfuko wa Barabara (Road Fund) ili



kuuwezesha kuwa na makusanyo yatakayowezesha ujenzi na ukarabati wa barabara Nchini.

Kirumba ameshauri hilo leo May 30,2024 wakati akichangia Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha 2024/25 ambapo ameanza kwa kushauri mfuko huo kubuni njia mpya ya upatikanaji wa fedha.

"Tumekuwa tukisaini barabara mpya kila kukicha barabara kongwe hazipitiki na naendelea kusisitiza Road Fund iangalie chanzo kipya tumeona katika bajeti ya taknolojia na habari walisema laini ambazo ziko active ni milioni 72 sasa ni wakati wa kuona kama ni katika kupitia chanzo cha simu tunaweza kupata kwa kila laini Tsh. 50 ili iweze kuisaidia Road Fund na hili inabidi tuongee ukweli tatizo la kiuzalendo na tunapoendelea mbele tuangalie tunaisaidiaje Road Fund"

Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page