![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_756aaafd8ff54b33b34f57ddad06c6fe~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_756aaafd8ff54b33b34f57ddad06c6fe~mv2.jpeg)
Mchekeshaji Aloma Isaac Junior (33) @zicsaloma kutoka Nigeria ametumia zaidi ya milioni 150 nchini Uturuki kufanya upasuaji (surgery) ya pua yake kwenye hospitali ya Istanbulrhinoplasty ya nchini Uturuki.
Mchekeshaji huyo anayefanya vyema mtandaoni Nigeria na nje ya mipaka ya taifa hilo ameishukuru hospitali hiyo kwa kumpatia pua ya ndoto yake. Wengi kupitia mitandao ya kijamii wamesema baada ya upasuaji huo mchekeshaji huyo amekuwa na mfanano na Hayati Michael Jackson. Baadhi ya wasichana wamesema wanamsubiri mwigizaji huyo arudi nchini kwao wakitamani wafunge nae ndoa.
Comments