top of page
Radio on air

MCHEKESHAJI SHAFII BRAND AFIWA NA MAMA YAKE MZAZI..

Mchekeshaji Shafii Brand aliyejizolea umaarufu kupitia vichekesho kwenye mitandao ya kijamii amefiwa na Mama yake mzazi kupitia ukurasa wake wa Instagram ameeleza taarifa hizi


"RIP MAMA YANGU

umeniacha wakat mgumu sanaaa mama angu dah sijakuangalia hata wakati unaniacha dah

NDO KWANZA SANAA IMEANZA KULETA MATUNDA MAMA ANGU ANAFARIKI JMN mengi huwenda sijakutendea na haikuwa bahati pumzika mama angu takuona tena MISEMO YOTE NILIKUWA NATUMIA KWENYE UCHESHI WANGU WW NDO CHANZO NASHUKUR SANA pumzika mama".

Msanii Beka Flavour amempa Pole Shafii akisema

"Pole sana ndugu yangu @shafii_brand kwa kumpoteza mama yako mzazi, Mungu akupe nguvu katika kipindi hiki kigumu, nakumbuka mara ya kadhaa tulikua tukiongea ulikua unanambia mama yetu ni shabiki mkubwa sana wa mziki wangu alikua anaziimba karibu nyimbo zangu zote nikakwambia nataka nije kumtembelea mama ukasema anaumwa yuko mwanza dah leo amekuacha mwenyewe pole sana nduguw yangu" ameandika @bekaflavour1


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page