top of page

MCHEKESHAJI TX DULLAH ANUNUA NDINGA SUBARU...

Mchekeshaji maarufu kwenye mitandao ya Kijamii TX Dullah ameonesha ni kwa namna gani ukitumia vyema kipaji ulichobarikiwa inalipa, kikubwa kikiwa ni ubunifu na kujituma.

Mchekeshaji huyu msomi wa Chuo Kikuu aliamua kuweka fani aliyoisomea pembeni na kujikita kwenye uchekeshaji mtandaoni kisha baadae kwenye majukwaa ya Stand Up Comedy na sasa ameanza kufaidi matunda aliyoyapanda kwa tabu.

Leo hii kupitia ukurasa wake wa Instagram ameonesha gari mpya aina ya Subaru aliyoinunua na kuandika "My New Shoe Txsubaru" ambapo chini ya chapisho lake hilo amepokea pongezi kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo watu maarufu na mashabiki zake kwa ujumla. Baadhi ya watu waliompa pongezi ni pamoja na @ndaro_ aliandika


"KARIBU SHELI FAMILIA LAZIMA WAELEWE NINI MAANA YA COMEDY TANZANIA"

Mtangazaji @noe_thefuture aliandika "Ungekua mwalimu mpk saivi hata baiskeli usinge kuwa nayo (Kidding) hongera sana kijana @txdullah" Nae Boss wa Cheka Tu @coy_mzungu alisema "Expert keep winning my guy! @txdullah" Nae @madirishatz Alicomment

"TRUST THE PROCESS

Hongera TxSubaru" Mchekeshaji @eliudsamwel nae alitoa pongezi

"Hongera kwa kununua gari Abdallah" @thekingkaka "Kubwaaaaa" Mchekeshaji @chard_talent nae alisema

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page