top of page

MCHEZAJI MTANZANIA CLARA LUVANGA ATIMIZA NDOTO YAKE YAKUKUTANA NA CR7 RONALDO...

Bila shaka kila mtu ana ndoto yake maishani ambayo anatamani siku moja aweze kuitimiza kama ilivyokuwa kwa mwanadada Clara Luvanga Binti wa Kitanzania anayecheza soka la kulipwa kunako klabu ya Al Nassr ya Nchini Saudi Arabia ambaye hii leo ametimiza ndoto yake ya kukutana na Binadamu mwenye wafuasi wengi duniani kwenye mtandao wa Instagram na



gwiji la soka Cristiano Ronaldo CR7.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram Clara ameweka wazi furaha yake kukutana na nyota huyo wanaecheza timu moja tofauti ni kwamba Ronaldo anacheza upande wa timu ya Wanaume na Clara anacheza upande wa timu ya Wanawake.

Kupitia ukurasa wa Clara ameandika ujumbe huu baada ya kukutana na Ronaldo kisha kupata picha ya pamoja wakiwa wameshikana mkono

"Ilikuwa ndoto kukutana nae na kupiga picha hatimae ndoto yangu imetimia Nina furaha sana kukutana nae" ameandika Clara.

Haya sasa Wanyarukoro wa Iringa binti wa nyumbani hii picha bango lake tuweke wapi Kihesa, Frelimo, Ipogolo, Mshindo, Miyomboni, Ilula, Kilolo, Gangilonga, Kalenga, Mafinga au Mtwivila?

Commentaires


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page