Mchezaji wa zamani wa Arsenal Thierry Henry amefunguka haya ,"Ushangiliaji wa Cristiano Ronaldo ni wa kuchukiza sana! Ikiwa ungetazama bao lake la mwisho dhidi ya Poland, ungeona kwamba Leão alifanya kazi na juhudi zote, akimpasia mpira mbele ya lango, na akafunga tu!
"Jambo la kawaida lingekuwa kwenda kwa Leão na kumshukuru angalau, lakini badala yake, alikimbia kushangilia kana kwamba lilikuwa bao la kwanza alilofunga katika maisha yake ya soka!
"Anahitaji kuelewa kuwa mabao mengine yanastahili kusherekea, na mengine hayafai. Angalia Lionel Messi alipofunga kwenye fainali ya Kombe la Dunia ambalo ni kinara wa soka, ungemuona akiwa ametulia akielekea kwa wachezaji wenzake ili kuwatia moyo zaidi! Mtazamo ni tofauti kabisa, na ndiyo maana Messi ni bora," anasema Thierry Henry.
Comments