top of page

MCHEZO WA KARNE: REAL MADRID DHIDI YA MANCHESTER CITY – NANI ATAFUZU 16 BORA?

Na Ester Madeghe


Jiji la Madrid linaenda kuwaka moto! Usiku wa leo, macho ya wapenda soka ulimwenguni kote yatakuwa yamelenga moja kwa moja Uwanja wa Santiago Bernabéu. Ni hatima ya vigogo wawili wa soka barani Ulaya – Real Madrid dhidi ya Manchester City. Hakuna cha huruma, hakuna nafasi ya makosa! Mwamuzi Istvan Kovacs anatarajiwa kuwa na usiku mgumu wa kuamua hatma ya miamba hawa katika safari ya kutinga hatua ya 16 bora ya Ligi ya Mabingwa huko barani ulaya


Baada ya mchuano wa kwanza uliomalizika kwa Manchester City kupoteza kwa mabao 3-2 katika dimba la Etihad, sasa ni zamu ya Real Madrid kucheza mbele ya mashabiki wao waaminifu. Pep Guardiola na Carlo Ancelott kilichopo kichwani kwa kila mmoja ni – KUSHINDA! Na vinginevyo


VITA YA NYOTA WA SOKA!


Hili siyo tu pambano la vilabu, bali ni vita ya mastaa wakubwa wa dunia!


Kwa upande wa Real Madrid, Kylian Mbappé, Vinícius Jr, na Jude Bellingham wanachora ramani ya ushindi, wakitafuta goli kila sekunde inapopita. Kwa upande wa Manchester City, jicho lote limeelekezwa kwa "mnyama wa magoli" Erling Haaland, anayesimamiwa na "mkono wa dhahabu" Kevin De Bruyne na "mchawi wa pasi" Phil Foden. Mbali na hao, majina mapya kama Omary Marmoush yanawasha moto wa matumaini ya kuleta mshangao usiku wa leo.


HISTORIA YA MWISHO ILIKUWAJE?


Mchezo wa kwanza ulikuwa wa kipekee! Dakika ya 19, Haaland alitumia mwanya kufungua karamu ya mabao kwa Man City. Real Madrid hawakukubali kupitwa – Mbappé alisawazisha dakika ya 60. Dakika ya 80, Haaland tena alipachika bao la pili kwa mkwaju wa penati, lakini Real Madrid wakajibu haraka – Brahim Diaz alisawazisha dakika ya 86. Lakini hakukuwa na mapumziko kwa Man City, kwani Jude Bellingham aliandika historia kwa bao la dakika za mwisho lililowavunja moyo mashabiki wa City.


KIFO NA KUZALIWA KWA NDOTO ZA UBINGWA!


Mchezo wa leo si wa kawaida – ni mapambano ya kufa au kupona! Ushindi unamaanisha tiketi ya 16 bora, na kushindwa ni ndoto kufa kabla ya muda wake. Tayari vigogo kama FC Barcelona, Arsenal, Liverpool, Aston Villa, Inter Milan, Atletico Madrid, Bayern Leverkusen, Lille, Feyenoord, Club Brugge, Bayern Munich na Benfica wameshafuzu.


Swali linabaki:

Je, ni nani atakayeandika jina lake kwenye orodha hii ya matajiri wa Ligi ya Mabingwa barani ulaya

Real Madrid au Manchester City?


Usiku wa leo, historia mpya itaandikwa!

Je ni dakika 90 au 120 zitaamua kumpeleka mmoja katika 16 bora

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page