top of page

MCHUNGAJI AKUTWA NA VIUNGO VYA BINADAMU KWENYE GARI LAKE KENYA, MWOSHA MAGARI NDIE AFICHUA HILO..Na VENANCE JOHN

Maafisa wa Polisi wanamshikilia mtu aliyejitangaza mwenyewe kama mhubiri ambaye amekutwa akimiliki sehemu za viungo vya binadamu ndani ya gari lake ambavyo vimetambuliwa na muosha magari.

Mtuhumiwa ametambuliwa kama Levis Simiyu ambaye anasemekana kuwa mchungaji wa



kanisa katika eneo la Ndivisi.

Maafisa kutoka Webuye Mashariki wamesema kwamba viungo hivyo vya mwili vilikuwa vimefichwa kwenye boksi.

Muosha magari huyo alikuwa anasafisha viatu vya mteja wake ndipo akagundua mguu wa mtu ambao umetokeza ukionekana kama uliounguzwa na kuwekwa juu ya viungo vingine.

Kijana huyo baada ya kuona hivyo, aliacha jukumu lake la kuendelea na usafi, kisha kumtaarifu boss wake na kuliangalia boksi hilo.

Mkurugenzi wa upelelezi wa makosa ya jinai amesema baadaye polisi waliitwa eneo la tukio.

Meneja wa kituo cha kuosha magari haraka baada ya kujuzwa na kijana wake aliyekuwa anasafisha gari hilo juu ya uwepo wa viungo vya binadamu kwenye gari la mteja aliyekuja kusafisha gari, meneja huyo haraka aliwataarifu polisi wa kituo cha Webuye ambao walifika haraka kabla ya mmiliki wa gari hajaondoka.

Viungo hivyo vimepelekwa katika makafani (mortuary) ya hospitali ya Webuye kwa ajili uchunguzi zaidi.

Commentaires


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page