top of page

MCHUNGAJI ALIYEMWITA RAIS PEPO AACHIWA HURU NCHINI GUIENEA YA IKWETA...Na VENANCE JOHN

Mchungaji na waziri wa zamani wa sheria wa Guinea ya Ikweta, ambaye alifungwa miaka miwili iliyopita kwa kumwita rais pepo, ameachiwa huru.

Rubén Maye Nsue Mangue ameachiwa huru baada ya kusamehewa na Rais Teodoro Obiang Nguema.

Bw Mangue alikamatwa kwa kumkosoa Rais katika kanda ya sauti iliyosambazwa sana



mitandaoni mwaka wa 2022, akimuita rais pepo kwa kuwa alikuwa amewashikilia watu wa Rubén Maye Nsue Mangue.

Rais Obiang mwenye umiri wa miaka 82, ndiye mtawala aliyekaa madarakani kwa muda mrefu zaidi barani Afrika, baada ya kuchukua mamlaka na madaraka kupitia mapinduzi ya mwaka 1979 ambapo mpaka sasa bado ni rais.

Bw Mangue baada ya kukamatwa alikataa kuomba msamaha hatua ambayo ilimfanya kufunguliwa mashtaka kwa kuchochea ghasia za umma huku wizara ya haki pia ikamfungia kuhubiri.

Bw Obiang ametajwa na mashirika ya kutetea haki za binadamu kuwa mmoja wa viongozi wakiimila barani Afrika.

alishinda muhula wa sita katika uchaguzi wa 2022, kwa takribani 95% ya kura.

Bwana Mangue ni mchungaji wa Kipentekoste aliyetawazwa rasmi, kuhudumu katika Kanisa la Prophetic Ministry of the Shadow of Christ na alikuwa waziri wa sheria kuanzia 1998 mpaka 2004 alipofutwa kazi kufuatia tofauti kati yake na rais.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page