top of page

MCHUNGAJI MALISA AFUKUZWA CCM KISA ALIPINGA RAIS SAMIA KUPITISHWA KUWA MGOMBEA PEKEE URAIS 2025

Na VENANCE JOHN


Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro, kimemfukuza uanachama kada wa chama hicho Mchungaji Godfrey Malisa kuanzia leo Februari 10, 2025 kwa tuhuma za kukiuka Katiba na maadili ya Chama hicho. Hatua ya kufukuzwa kwa Mchungaji Malisa imeelezwa kuwa inatokana na kauli alizokuwa akizitoa kupinga uamuzi wa Mkutano Mkuu wa CCM Taifa wa Januari 19, 2025.


Taarifa zinadai kuwa, kada huyo alidai kupitisha kwa wagombea hao (Rais Samia Suluhu Hassan kwa upande wa Tanzania Bara na Dr. Hussein Mwinyi kwa upande wa Tanzania Zanzibar kumekiuka Katiba ya CCM.


Mchungaji Malisa, ambaye amewahi kugombea nafasi ya urais, uspika na hata ubunge, alijiunga na chama cha CCM mwaka 2021 na alikuwa miongoni mwa makada 9 waliochukua fomu kugombea uenyekiti wa Chama hicho mwaka 2022.


Leo Katibu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro, Merce Mollel amesema uamuzi huo umefikiwa kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM ya mkoa. Kwa mujibu wa tovuti ya gazeti la Mwananchi, Dr Malisa hajahusishwa wala hakupewa taarifa na chama chake juu ya maamuzi hayo.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page