Na Godson Mbilinyi
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ACP Muhudhwari R. Msuya ambaye ni Kaimu Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Pwani inaeleza kuwa

"Tarehe 27.10.2024, majira ya saa 21:15 Usiku huko Simbani, Wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani mwanamke mmoja, Veronica Riwa, Miaka 77, Mkristo, Mfugaji na mkazi wa Simbani, alikutwa nyumbani kwake akiwa ameuwawa kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali kichwani.
Uchunguzi wa awali umebaini kuwa aliyefanya mauaji hayo ni mchungaji wa ng'ombe wa marehemu na baada ya tukio hilo mtuhumiwa alitoroka na juhudi za kumtafuta zinaendelea ili hatua za kisheria zichukuliwa dhidi yake
Aidha Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linatoa wito kwa wananchi kutoa ataarifa kwa viongozi wa mitaa yao juu ya watu wanaoishi nao wakiwa ni wasaidizi wa kazi mbalimbali za nyumbani ili kusaidia kuwatambua kirahisi yanapotokea matukio ya kijinai na kimaadili ili wachuliwe hatua stahiki."
Comments