top of page

MECHI YA LIGI KUU YANGA DHIDI YA DODOMA JIJI ITAKUWA NI GAMONDI DAY - ALLY KAMWE

Akizungumza na waandishi wa habari Afisa Habari wa Yanga SC Ally Kamwe ametoa taarifa kuwa

"Kesho tunasafiri majira ya saa nne asubuhi kuelekea pale mkoani Dodoma kucheza dhidi ya Dodoma Jiji. Mchezo huo utafanyika tarehe 22 Mei 2024. Mechi hii ya Dodoma tumeifanya mechi ya kushukuru benchi la ufundi. Hivyo itakuwa ni GAMONDI DAY




Kwenye GAMONDI DAY itakapofika dakika ya 30, wana Yanga wote tunapaswa kusimama kumpigia makofi Gamondi na benchi lake la ufundi kwa dakika moja. Tunampa heshima Gamondi kwa kutupatia ubingwa wa kishitoria mara ya 30" @alikamwe

Ally Kamwe ameongeza kuwa shabiki kama unaweza kunyoa kipara nyoa, au uje na picha ya Gamondi siku hiyo.

"Kwenye GAMONDI DAY ukiweza kupiga dongo kama Gamondi wewe piga uje kumpongeza Masta Gamondi. Ametuheshimisha sana, Yanga Bingwa na ushindi mnono wa Magoli 7 kwenye Derby

Ukiweza kutengeneza picha ya Masta Gamondi, njoo na picha yake uwanjani. Kama unaweza kubeba bango lenye ujumbe wowote njoo nalo. Kwa mfano unaweza kubeba bango limeandikwa Masta Gamondi kiboko wa mayi wetu" @alikamwe


Commentaires


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page