Swaggy Daddy ambaye ni Meneja wa msanii wa Bongo Fleva Jux amemuandikia ujumbe huu msanii wake baada ya kufunga ndoa hapo juzi. @swaggdaddyyoungray ameandika
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_d9e86c9903e8418d81406951d4668445~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_d9e86c9903e8418d81406951d4668445~mv2.jpeg)
"My brother @juma_jux C, officially stepping into this new journey of #JPs2025! Naomba Mwenyezi Mungu awe nanyi, akufungulie milango ya baraka, na hii iwe chachu ya kuanzisha familia bora na yenye mafanikio. Safari hii ni kubwa, na najua itakuwa moja ya hatua muhimu zaidi kwenye maisha yako na mwenza wako Bi Khadiza @its.priscy.
Takriban miaka 15 ya urafiki na kazi pamoja, hatujawahi kugombana wala kupishana! Heshima, uaminifu, na utu vimetutangulia kabla ya chochote. Tumeanza kama marafiki, leo tuko kama ndugu wa damu! Dunia hii imejaa changamoto, hasa inapokuja kwenye kazi na pesa, lakini kwetu sisi utu umekuwa kipaumbele. Kwa hili, linanipa imani kubwa kuwa wewe utakuwa kiongozi bora wa familia yako C.
Naomba nikushukuru leo tena, Asante kwa kuniamini na kunipa nafasi kubwa katika maisha yako. Kuwa meneja wako si kazi tu, ni dhamana kubwa sana. Wengi hawajui, lakini msanii hufuata ushauri wa meneja wake kwa asilimia 80-90, si tu kwenye muziki, bali hata kwenye maisha yake binafsi. Hii nafasi siyo ya mchezo, inahitaji busara, uvumilivu, na hekima kubwa. Naahidi kuwa bega kwa bega nawe kwenye kila hatua ya safari hii!
Juzi ilikuwa mara ya pili kukuona ukilia mbele ya watu, na kama ndugu yako, ilinigusa sana. Nimeona jinsi ulivyoipokea kwa furaha hii safari yako mpya, na najua hii hatua mpya ina maana kubwa sana kwako. Kwa lolote linalokufurahisha, najua litani furahisha pia, na lolote linalokugusa na kukuumiza, litani gusa na kuniumiza mimi pia.
Mwenyezi Mungu akutangulie, akupe baraka zaidi, na safari hii iwe ya amani, upendo, na mafanikio! Nakutakia kila la kheri, ndugu yangu!"
Comments