Na VENANCE JOHN
Kampuni ya Meta jana imesema imekubali kulipa takribani dola milioni 25 kutatua kesi ya Rais Donald Trump juu ya kampuni hiyo kusimamisha akaunti zake baada ya shambulio la Januari 6, 2021 katika Ikulu ya Marekani.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_8042928281b2472e8dd31564785d8393~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_8042928281b2472e8dd31564785d8393~mv2.jpeg)
Trump alifungua kesi dhidi ya Twitter Inc, ambayo sasa inajulikana kama X, Facebook Inc iliyo chini ya kampuni mama ya (Meta) na Alphabet Inc inayoimiliki Google, pamoja na wasimamizi wao wakuu mwezi Julai 2021, kwa madai kwamba walinyamazisha maoni yake na wafuasi wake kinyume cha sheria.
Akaunti za Trump za Facebook na Instagram zilisitishwa baada ya wafuasi wake kushambulia Ikulu ya Marekani kufuatia hotuba yake akirudia madai ya uwongo kwamba kushindwa kwake katika uchaguzi kulitokana na udanganyifu ulitokea.
Kati ya kiasi hicho cha malipo, dola milioni 22 zitatumika kwa mfuko wa maktaba ya urais wa Trump, na zilizosalia kwa ada za kisheria na walalamikaji wengine katika kesi hiyo. Kampuni mama ya Facebook ambayo ni Meta iliwasilisha notisi kuhusu suluhu hiyo katika mahakama ya shirikisho huko San Francisco.
Comments