top of page

MGAHAWA UNAOENDESHWA KILA

MGAHAWA UNAOENDESHWA KILA

KITU NA ROBOTI ZINAZOONGOZWA

KWA Al WAFUNGULIWA CALIFORNIA

Na mwandishi wetu Nassor Nangi

CaliExpress by Flippy, mgahawa mpya uliofunguliwa huko Pasadena, Kusini mwa California Marekani umeripotiwa kutumia roboti kupika kila kitu, kuanzia baga hadi mikate, bila ya usaidizi


wa binadamu huku huduma zote za mgahawani hapo unaweza kuzitazama mwenyewe na kuthibitisha roboti zikipika mlo wako mbele yako.

Biashara hii ya kiubunifu ni ushirikiano kati ya Cali Group, Miso Robotics, na PopID, ambayo imekuja kuleta mageuzi katika sekta ya migahawa huko Marekani.

Misosi inayopikwa haswa ni pamoja na burger, cheeseburger bila kusahau fries za Kifaransa.

Kulingana na John Miller, Mkurugenzi Mtendaji wa PopID, mgahawa huu utakua wa kwanza kimataifa kufanikisha shughuli za kuagiza huduma na kupika kiroboti bila ya usaidizi wa binadamu.

Chanzo: CBS (kupitia YouTube)

Je unatamani kupikiwa msosi gani na roboti?

Usiache kufuatilia Msasa Online kwa habari zaidi

コメント


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page