top of page

MICHELLE OBAMA ATANGAZA KUWA HATOGOMBEA URAIS 2024..


Kumekuwa na uwepo wa tetesi nyingi kuhusiana na mke wa aliyekuwa Rais wa Marekani Barack Obama, Michelle Obama kutaka kugombea Urais 2024, Sasa Michelle amekanusha tetesi hizo kupitia ofisi yake siku ya jana Jumanne Machi 5.

Ofisi hiyo imelithibitisha hilo kwa kueleza kuwa Michelle hatogombea Urais kwani kwasasa ameamua kujikita kumuunga mkono Rais Biden katika kampeni zake ili kufanikisha achaguliwe tena. Uchaguzi nchini Marekani unatarajiwa kufanyika Novemba 5, 2024, na mpaka sasa waliojitokeza kugombea Urais ni pamoja na Joe Biden ambaye yupo madarakani na Donald Trump.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page