top of page

MIPANGO ILIYOPO NI KUREJESHA MAKALI YETU - AHMED ALLY

Kutoka kwa Meneja habari na mawasiliano Simba SC Ahmed Ally amefunguka haya

"Tunaposhangilia @simbaqueensctz kuifunga Nyuma Mwiko Princess sio tunatafuta faraja bali



tunafurahi kuona Brand ya Simba Sports Club inalindwa

Kulinda Brand ya taasisi sio kwa kuomba Interview za watu zifutwe, Brand inalindwa kwa bidhaa za Taasisi kufanya vizuri

Timu yetu ya kikosi cha Wakubwa haina mwenendo mzuri kwa siku za hivi karibuni lakini haiondoi ukweli kuwa maendeleo ya taasisi yetu yanakwenda vizuri

Simba U 17 inafanya vizuri kwenye ligi ya vijana, Simba U 20 tume qualify kwenye nane bora na Simba Queens ndo hao wanakaribia kuwa mabingwa wa ligi ya Wanawake

Mipango iliyopo sasa ni kufanya uwekezaji mkubwa kwenye kikosi cha Wakubwa na kurejesha makali yetu ili taasisi yetu iwe na mafanikio katika idara zote

Zipo taasisi nyingine zimetelekeza bidhaa zao timu zao za Watoto ziko hovyo hata jezi hawana wanavaa jezi za wakubwa na kubandika plasta za Wanawake ndo tabaani

Inawezekana tukahukumiwa kwa mwenendo mbaya wa kikosi cha Wakubwa na ikaonekana hakuna kinachofanyika lakini ukweli kuwa taasisi iko imara sana na kikosi cha Wakubwa punde kitarejesha makali yake" Ahmed Ally.

Commenti


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page