top of page

MJUKUU AIBA HATI AUZA NYUMBA MILIONI 5, AMWACHA MJANE KWENYE MAJONZI

Ripoti kutoka Mtaa wa Sulungai Kata ya Ipagala, jijini Dodoma, Elizabeth Sudai (80) ameiomba serikali kumsaidia kupata nyumba yake ambayo imeuzwa baada ya mjukuu wake kuiba hati na kuiuza.


Akizungumza na waandishi wa habari kwenye nyumba hiyo inayodaiwa kuuzwa mwaka jana akiwa safarini kuuguza mgonjwa kijijini kwao, Elizabeth alisema aliporudi alikuta mjukuu ameiuza kwa Sh milioni tano kwa mtu anayedaiwa kuwa mtumishi wa serikali.


"Mimi sikuwepo nyumbani, nakuja naambiwa kuna mtu amenunua nyumba yangu na ameuziwa na mjukuu ambaye aliiba hati na nyaraka zingine na kufanya biashara kinyemela," alisema bibi huyo ambaye ni mjane.


Alisema alikwenda polisi na kufungua kesi ambayo mjukuu alikamatwa pamoja na aliyeuziwa nyumba. "Lakini kutokana na kubaini kuwa mjukuu wangu ndiye alikuwa na makosa, ikabidi polisi, mimi pamoja na mnunuzi kufanya makubaliano upya na kukubaliana iuzwe kwa Shilingi milioni 45, hivyo mnunuzi alipaswa kulipa kiasi kingine kilichobakia," alisema.


Alisema baada ya makubaliano hayo, kiasi kilicholipwa ni Sh milioni 10 pekee na nyingine hazijalipwa hadi sasa.


Credit to : Habari Leo

Commenti


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page