top of page

MKALI WA FILAMU NCHINI INDIA, SEIF ALI KHAN ADUNGWA KISU NYUMBANI KWAKE, AFANYIWA UPASUAJI

Na VENANCE JOHN


Muigizaji maarufu wa Bollywood Saif Ali Khan amefanyiwa upasuaji baada ya kudungwa kisu na mtu aliyeingia nyumbani kwake. Taarifa kutoka kwa watu wake wa karibu zinasema kuwa nyota huyo hayuko tena katika hatari baada upasuaji kufanyika salama.


Shambulio hilo limetokea mapema ya leo Alhamisi asubuhi katika mji wa Mumbai nchini India, ambapo Khan anaishi na familia yake. Polisi wa jiji wamesema kwamba mwigizaji huyo amejeruhiwa baada ya ugomvi kuzuka kati yake na mtu asiyejulikana ambaye aliingia nyumbani kwake muda wa saa sita usiku.


Baada ya mkasa huo, tayari polisi wameunda timu ya kuchunguza suala hilo. "Khan ametoka kwenye upasuaji na hayuko ktika hatari. Kwa sasa yuko kwenye ahueni na madaktari wanafuatilia maendeleo yake," timu ya Khan imesema katika taarifa yake.


Akizungumza na waandishi wa habari baada ya upasuaji huo, Dk Nitin Dange wa Hospitali ya Lilavati, ambako Khan amelazwa, amesema kuwa mwigizaji huyo alipata jeraha kubwa kwenye uti wa mgongo wa kifua kutokana na kudungwa kisu kwenye uti wa mgongo.


"Upasuaji ulifanyika ili kutoa kisu na kurekebisha maji ya uti wa mgongo yaliyovuja. Majeraha mengine mawili ya kina kwenye mkono wake wa kushoto na jingine shingoni yalirekebishwa na timu ya upasuaji wa urembo (plastic surgery)," amesema Dr. Nitin Dange. Maelezo kamili ya shambulio hilo bado hayajabainika.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page