top of page

MKE WA GSM AJENGA MSIKITI WENYE THAMANI YA MILIONI 600 KAMA ZAWADI BIRTHDAY YA MUMEWE

Kutoka Dodoma Madame Salha ambaye ni Mke wa Mfanyabiashara Ghalib lSaid Mohamed (GSM) ameanza ujenzi wa Msikiti na Madrasa zenye thamani ya Tsh Milioni 600 katika eneo la Kibaigwa, Kongwa, Dodoma ikiwa ni zawadi aliyoitoa kusherehekea mfanano wa siku ya kuzaliwa ya Mume wake November 19.


Rais wa Yanga Injinia Hersi Said ambaye aliambatana na GSM na Mke wake, amewaambia Wakazi wa Kibaigwa, Kongwa na Dodoma kwa ujumla kwamba chanzo cha ujenzi huo ni Madam Salha "wakati akifikiria jinsi gani atasherehekea siku hii maalum kwa Mume wake akakusanya maoni mbalimbali, tayari alikuwa ameweka dhamira ya kumjengea Mr. Ghalib Msikiti utakaobali katika maisha yake na baada ya kuondoka katika ardhi hii"


Mfanyabiashara Ghalib pamoja na biashara zake nyingine, ni Mdhamini na Mfadhili wa Club ya soka ya Yanga.

コメント


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page