Kampuni ya Achimwene Safari imefanikiwa kushinda tuzo ya Msafirishaji Bora na Salama Mwaka 2023/24 kwenye tuzo za Mamlaka ya udhibiti usafiri ardhini kwa wenye Mabasi 3 hadi 10 kama mshindi namba 2 ambapo kampuni imetunukiwa tuzo.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_9a8172c70ada46f9b10d3aca9268d432~mv2.jpg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_9a8172c70ada46f9b10d3aca9268d432~mv2.jpg)
Tuzo hiyo imepokelewa na Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Heneriko Achimwene @achimwene_business , Meneja wa Kampuni Innocent Mbeyela @innocent.mbeyela Pamoja na wafanyakazi wawili Sophia Laizer na Hans.
Tuzo hizo zimetolewa mbele ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Isdor Mpango katika ufunguzi wa wiki ya Nenda kwa Usalama viwanja vya Jamhuri jijini Dodoma. Achimwene imepongezwa Kwa kutoa Huduma Bora na Salama na imesisitizwa kuendelea kufanya hivyo ambapo uongozi umeahidi kuendelea kutoa huduma bora.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_ef33e949975a47ec87e925875208dc31~mv2.jpg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_ef33e949975a47ec87e925875208dc31~mv2.jpg)
コメント