top of page

MKUU WA MAJESHI YA ULINZI KENYA KUZIKWA JUMAPILI APRILI 21...




Kutoka nchini Kenya Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Francis Ogolla ambaye amefariki katika ajali ya Helikopta ya Jeshi iliyotokea jana Aprili 18, 2024 baada ya kupaa kutoka eneo la Kaben, Marakwet taarifa ya familia imeeleza kuwa inatarajia kuwa Marehemu atazikwa Jumapili Aprili 21 katika makazi yake huko Ng'iya, Alego Usonga, Kaunti ya Siaya.

Siku ya jana Rais William Ruto alitangaza kifo hicho na kueleza, mbali na CDF Ogolla aliyechukua nafasi hiyo Aprili 28, 2023, wengine waliokuwa kwenye Helikopta hiyo ni Maafisa kadhaa wa Jeshi ambao nao wamepoteza maisha

Rais Ruto alimpandisha cheo Luteni Jenerali Francis Omondi Ogolla kuwa Jenerali na kumteua kuwa CDF akichukua nafasi ya Jenerali Robert Kariuki Kibochi aliyemaliza muda wake.



Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page