Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Mohamed Mchengerwa kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan anasikitika kutangaza kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Mbozi Mhe. Ester Mahawe kilichotokea leo tarehe 14.01.2025 kwenye Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Kaskazini mkoani Kilimanjaro alipokua akipatiwa matibabu. KCMC
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_85e01d87c9be4b04aa2bb7190d39c9a8~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_85e01d87c9be4b04aa2bb7190d39c9a8~mv2.jpeg)
"Nimepokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Mbozi mkoani Songwe Mhe. Ester Mahawe. Kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ninatoa pole kwa familia, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, wafanyakazi na wananchi wote wa wilaya ya mbozi, ndugu, jamaa na mafariki kwa msiba huu. Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi' amesema. Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kushirikiana na familia inaendelea kuratibu shughuli za mazishi na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE. Aidha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za pole kupitia ukurasa wake wa Instagram
"Nimepokea kwa masikitiko taarifa za kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Mbozi, Mkoa wa Songwe, Bi. Esther Alexander Mahawe, kilichotokea leo tarehe 14 Januari, 2025 katika hospitali ya KCMC, mkoani Kilimanjaro. Nawapa pole familia ya marehemu, Mkuu wa Mkoa wa Songwe, ndugu, jamaa na wote walioguswa na msiba huu.
Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa maisha ya Bi. Esther na utumishi wake kwa umma ambao uliongozwa na uchapakazi hodari, ukweli na msimamo thabiti katika utendaji. Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi.
Amina."
Comments