top of page

MKUU WA ZAMANI WA GOOGLE AONESHA HOFU YAKE KWA AKILI MNEMBA (AI)

Na VENANCE JOHN


Mkurugenzi mkuu wa zamani wa Google, Eric Schmidt amesema anahofia kwamba taarifa za kijasusi za Akili Mnemba (artificial intelligent) zinaweza kutumiwa na magaidi au watu matapeli kuwadhuru watu wasio na hatia. Eric Schmidt amesema hofu halisi aliyo nayo sio ile ambayo watu wengi huzungumza kuhusu akili mnemba (AI) akisema yeye anazungumza juu ya hatari kubwa.


Bilionea huyo wa teknolojia, ambaye alishikilia nyadhifa kuu katika Google kutoka 2001 mpaka 2017, leo amesema Korea Kaskazini, au Iran, au hata Urusi inaweza kupitisha na kutumia teknolojia hiyo vibaya kuunda silaha za kibaolojia.


Eric Schmidt ametoa wito wa serikali kuwa waangalizi kwa kampuni za kibinafsi za teknolojia ambazo zinaunda miundo ya akili mnemba (AI), lakini akaonya kuwa udhibiti wa kupita kiasi unaweza kukandamiza uvumbuzi.


Bw Schmidt aamesema inatikiwa kuwapo udhibiti wa mauzo ya nje ya Marekani kwenye microchips zenye nguvu ambazo zinatumia mifumo ya hali ya juu zaidi ya akili mnemba (AI). Kabla ya kuondoka madarakani, Rais wa zamani wa Marekani Joe Biden alizuia usafirishaji wa microchips kwa nchi zote isipokuwa 18, ili kupunguza maendeleo ya wapinzani kwenye utafiti wa akili mnemba.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page