top of page

MLIPUKO WA BAKTERIA WA E. KOLI (ESCHERICHIA COLI) KATIKA KAROTI WAUA MTU 1 NA WENGINE KADHAA KUUGUA KOTE MAREKANI

Na VENANCE JOHN


Vituo vya Marekani vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) vinachunguza mlipuko wa bakteria anayejulikana kama E. koli (Escherichia coli) katika angalau majimbo 18 yanayohusishwa na baadhi ya karoti zinazolimwa bila kutumia mbolea na viuatilifu ya viwandani kusababisha angalau kifo kimoja.


Kulingana na CDC angalau kesi 39 za E. koli (Escherichia coli) zimehusishwa na karoti tangu mwezi Septemba, na kusababisha kulazwa hospitalini watu 15 na kifo kimoja, Kesi za E. koli zilizoripotiwa zimehusishwa na aina nyingi za chapa za watoto wachanga na karoti za watu wazima


Zilizoombwa kurerejeshwa kwa mzalishaji, ambaye ni kampuni ya Grimmway Farms, mzalishaji wa karoti aliye na makao yake makuu huko Bakersfield, jimboni California. Grimmway Farms inasema timu yake ya chakula na usalama sasa inafanya kazi na wauzaji na mamlaka ya afya ili kukabiliana na milipuko hiyo.


"Tunachukua jukumu letu katika kuhakikisha usalama na ubora wa bidhaa zetu kwa umakini," Rais na Mkurugenzi Mtendaji wa Grimmway Farms Jeff Huckaby alisema katika taarifa. "Afya ya wateja wetu na uadilifu wa bidhaa zetu ni vipaumbele vyetu vya juu, na tunafanya mapitio ya kina ya mbinu zetu za upandaji, uvunaji na usindikaji."


Watoto walio na umri wa chini ya miaka 5, watu wazima wenye umri wa miaka 65 au zaidi na wale walio na kinga dhaifu wako kwenye hatari kubwa ya kuambukizwa, CDC imesema. Wateja wameshauriwa kwamba wanapaswa kumpigia simu mhudumu wa afya iwapo watapata dalili kali za E. koli, ikiwa ni pamoja na kuhara, homa, kutapika na kizunguzungu.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page