top of page

MNAHISI NIMETOKA FAMILIA YA KITAJIRI

Muigizaji Idriss anatupitisha kwenye historia ya maisha yake kama ulikuwa unadhani anatokea familia ya kitajiri basi majibu haya hapa Kuna watu huwa mnahisi nimetoka katika familia ya kitajiri kisa nimejirltahidi kakiingereza kidogo na nimeanzia umaarufu kwenye show ya kiingereza Africa. Siwalaumu.


Naitwa Idris Sultan, nimezaliwa Mount Meru hospitali Arusha. Nimekulia Arusha, nimeishi nyumba za Kotaz kilombero Ngarenaro. Nimesoma Arusha Sec maarufu kama seki. Tulifungiwa kushiriki mashindano ya michezo sababu tulifungwa nusu fainali tukapasua matairi ya coaster la walioshinda. Labda ndo maana matege yamekosa kazi maalum kisoka.


Nimemaliza jeshi 2012 nikafaulu kuingia Muhimbili na ka-PCB kangu ka kuunga ila hela ilikuwa ngumu sana mdogo wangu anahitaji kusoma na mama mishe hazitiki freshi nikawa kibarua Iview studios kama mtu wa kutafuta mamodo wa matangazo sababu nilikuwa najuana na wengi facebook ila haikulipa nikaanza jifunza photography nikawa photographer kisha graphic designer.


Nikiwa head of photography nikaona nafasi ya kuingia BBA nikajichomeka sielewi hili wala lile mwana likatiki mimi nikapanga na wafanyakazi wenzangu nikae BBA mwezi tu nipate umaarufu tupate kazi zaidi ila kwa bahati mbaya nikashinda. Kuanzia hapo story ina majonzi kidogo vuta kiti. Mwana nilipoteza 600M ndani ya mwaka mmoja sababu ya ushkaji ushkaji (hii tazama Salama na Idris Youtube).


Nikakumbuka kwani hela zimechomwa au zipo mikono ya watu wengine? Nazipataje? Ujuzi ninao, vitendea kazi ninavyo. Nikaanza kuchapa graphics za maana na proposal makampuni 100 yanatiki mawili. Nikapata kazi choice fm nikawa na hela za bajaji. Ile zipu imesaidia kulinda kijiheshima. Wakatu huu nimepewa chumba nana kaka angu Max pale mbezi nimenunua feni yangu 90k saaafi siwezi alika bebez kwa watu kwahiyo nimehifadhi sana hasira chini mkanda kama mfungwa vile.


Makampuni mengine yakaanza kuona kazi, nikaanza kuokota. Nikapangisha chumba, mambo yakajipa zaidi nikavuta nyumba nyingine. Nikajifunza kuandika scripts, shooting film & editing. Kwa ule ujuzi wa photography hili halikuwa ishu sana nikaanza kuwapa Stafu, Danga, Redio. Wana mkasema nina kitu mkanipa kichwa nikawavamia Netflix na script yangu wakatiki. Mkasema nina spidi sana mkaniweka ndani na makesi ya mahakamani kidogo mniue nyie. Mkaniachia nikafunguka kama kiberenge.


Sasahivi maza yupo zake na shamba lake anakula private life mdogo mdogo najaribu kutimiza ndoto zake huku nikipambania Oscar na hollywood zangu.

Ila tupo hapa tunasema nina zero battle ground. Ehhhh MABIGIIIIII."

コメント


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page