MREMBO VANNYBRAD AWAACHA WATU MIDOMO WAZI BAADA YA KUMMWAGA

MZUNGU NA KUDAI TALAKA...
Imekua gumzo mitandaoni huko nchini Kenya, baada ya video ya mtayarishaji maudhui wa mtandaoni maarufu kwa jina la Vanny, akionekana kucheza kwa ajili ya mume wake mzungu kuibuka muda mfupi baada ya kutangaza kuwa wameachana.
Haijulikani kwa nini mrembo huyo amechagua kumwacha mume wake, na alipokuwa akitangaza kuachana kwao alisema waliachana kwa amani.
Tetesi zao za kuachana zilianza miezi kadhaa iliyopita, lakini wenzi hao walikuwa wamezima madai hayo kupitia video zenye mahaba zilizokuwa zikionesha ukaribu mzuri baina ya wanandoa hao.
Mwanadada huyo alichapisha ujumbe mfupi kupitia kwenye ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika maneno yenye kumaanisha kwamba, "Hujawahi kunisikia nikilalamika lakini safari hii nasikitika kusema kwamba mimi na Brad tumeachana rasmi kwa heshima na kwa njia nzuri ilikuwa ndoa nzuri sana lakini tofauti zetu na kila kitu kilichotokea kilichochea tu uhusiano kufika ulipofikia... Nawapenda nyote na wakati huu ningepumzika na kutoka kwenye mitandao ya kijamii hadi nitakapotangaza tena".
Comments