top of page

MSAFARA WA MKUU WA WILAYA BUSEGA WASHAMBULIWA KWA MAWE NA WAANDAMANAJI, 108 WAKAMATWA

Na VENANCE JOHN


Mkuu wa wilaya ya Busega mkoani Simiyu Faiza Salim, amesema waandamanaji wameshambulia msafara wake akiwa na viongozi wengine wakati alipokwenda kuwasikiliza waandamanaji hao.





Akizungumzia maandamano yaliyotokea Lamadi, leo agosti 21, 2024, Mkuu huyo wa wilaya ya Busega amesema athari zilizotokea ni baadhi ya Viongozi kushambuliwa kwa kupigwa mawe akiwemo yeye mwenyewe.


Waandamanaji walikuwa wakiandamana kufuatia taarifa kuwa watoto wanapotea ingawa Mkuu huyo wa wilaya amesema kwa muda wa miezi minne aliyokuwa katika nafasi hiyo hajapata taarifa ya watoto kupotea.


Faiza amesema mabomu ya machozi yamepigwa kwa kuwa walizuia magari yote na kuharibu miundombinu na maduka na walijaribu kuchoma kutoa na kuvunja vioo vya magari yaliyokuwa yanapita na kusema hilo hawawezi kulikibali wao kama mamlaka.


Juu taarifa za waandamanaji kupoteza maisha, amesema hajapokea taarifa kama kuna mtu aliyefariki, na kwamba inawezekana yapo majeraha madogo. Faiza Salim amesema mpaka sasa tayari watu 108 wameshakamatwa na watapelekwa mahakamani.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page