top of page

MSANII ZUCHU AOMBA RADHI KWA KOSA HILI

MSANII ZUCHU AOMBA RADHI KWA KOSA HILI

Kutoka kwa msanii Zuchu anayesimamiwa na lebo ya muziki ya WCB ya msanii Diamond Platnumz amefunguka ujumbe huu wa kuomba radhi

"KUOMBA RADH


Kwa Wapenzi Wetu wa Sanaa

Napenda kutumia fursa hii kuwaomba radhi kutokana na maneno niliyoyatumia kwenye kibwagizo ambacho kilileta taharuki kwenye tamasha la Full Moon Party - Kendwa Beach Zanzibar hivi karibuni.

Najua kuwa maneno yameleta sintofahamu kwa wengi wenu na kuleta maana hasi kwa jamii na mashabiki zangu kiujumla.

Nia yangu ilikuwa kuleta burudani njema na furaha kwa mashabiki wangu wote. Si lengo langu kupotosha, kumomonyoa maadili au kuleta taharuki kwa yeyote.

Ninachukua ahadi leo kufanya kazi na timu yangu ili kuhakikisha matukio kama hayo hayatokei tena kwenye matamasha yajayo.

Nawaomba radhi tena kwa jamii na Baraza la Sanaa (BASATA) ambao ndio walezi wangu.

Zuhura Othman Soud (Zuchu)

Mwanamuziki

Wasafi Limited."

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page