top of page

MSEMAJI WA IKULU YA MAREKANI AMALIZA UTATA JUU YA  BIDEN KUGOMBEA Na VENANCE JOHN

Baada ya uvumi kuenea kuwa Rais wa Marekani Joe Biden anaweza kujiondoa kwenye kinyang'anyiro cha kuwania muhula wa pili wa Urais, sasa ni rasmi kuwa atagombea.

Baada ya kufanyika kwa mdahalo dhidi ya Rais wa zamani ambaye pia anatarajiwa kuwa mpinzani wake kwenye uchaguzi huo Bw. Donald John Trump, kuliibuka mitazamo ya pande mbili, upande mmoja ukionesha wasiwasi kwani Joe Biden alionekana kushindwa kujibu vizuri maswali na wakati mwingine kushindwa kutoa sauti ya uhakika na isiyosikika vizuri huku


upande mwingine ukiendelea kumuunga mkono Biden na kuona kuwa ndiye anayetosha kupambana na Trump.

Baada ya kufanyika mazungumzo na uongozi wake wa kampeni, wamehitimisha kuwa Biden agombee.

"Nitagombea" amesema na kuongeza kwamba atabaki kuwa kiongozi wa chama cha Democrat.

Rais Biden alikutana na magavana wa Democrat ili kuwahakikishia lengo lake la kubaki katika mbio hizo licha ya kuanza kuibuka kwa maoni ndani ya chama chake  yanayomtaka kujiondoa kwenye mbio.

Ndani ya chama chake cha Democrat wapo wanaoona kuwa hatakiwi kuwa mpeperusha bendera ya chama hicho, huku kura za maoni zikipendekeza kuwa makamu wake Bi Kamala Harris kuchukua nafasi yake.

Katika mkutano na waandishi habari, msemaji wa ikulu Karine Jean Pierre alipoulizwa kama  Biden anafikiria kujitoa, amejibu"hakika hapana"

Hata hivyo mpaka sasa kura za maoni zinaonesha kuwa, Trump anaweza kumshinda Biden kwani Trump ana asilimia 48% dhidi ya 42% za Biden.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page