![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_e3a22f1290a94796a1836bccba03a7bb~mv2.jpg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_e3a22f1290a94796a1836bccba03a7bb~mv2.jpg)
Msemaji wa klabu ya Vital'O ya Burundi Arsene Bucuti amekutana na Msemaji wa Yanga SC Haji Manara ambapo ametoa ahadi nyingine kuelekea mchezo wa marudiano Ligi ya Mabingwa Afrika Jumamosi Agosti 24,2024 kwamba kama atafungwa tena kutolewa nje ya mashindano hayo basi atatoka kwa Mkapa kifua wazi mpaka katikati ya Jiji la Dar Es Salaam.
Aidha Manara pia amempa zawadi ya kumshonea Suti akifurahi kukutana nae na kubadilishana mawazo ya hapa na pale Ofisini kwake.
Source: Manara Tv
Comments