Na VENANCE JOHN
Mtalii wa ambaye ni raia wa Uhispania amefariki kwa kukanyagwa na Tembo baada ya kushuka kwenye gari lake na kupiga picha katika bustani huko Afrika Kusini karibu na mji wa Johannesburg.
Mtu huyo mwenye umri wa miaka 43 alipatwa na mkasa huo siku ya Jumapili asubuhi katika
![](https://static.wixstatic.com/media/146e6d_86fc661195cd451db7b5476d64ab38aa~mv2.jpg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/146e6d_86fc661195cd451db7b5476d64ab38aa~mv2.jpg)
Mbuga ya Kitaifa ya Pilanesberg.
Polisi wamesema mwanaume huyo ambaye alikuwa na wanawake wengine wawili walikuwa wakiendesha gari lao kwenye hifadhi na walipoona tembo watatu na watoto watatu wa tembo mwanaume huyo alishuka kisha kuanza kupiga picha.
Msemaji wa polisi Sabata Mokgwabone amesema ushahidi wa awali unaonesha kuwa mwanaume huyo alisimamisha gari, akatoka na akasogelea tembo hao ili aweze kupiga picha ndipo tembo walimvamia na kumuua.
Pieter Nel, meneja wa uhifadhi katika Mamlaka ya Hifadhi na Utalii ya Mkoa wa Kaskazini Magharibi, amesema Tembo huyo alipandwa na hasira alipomwona mwanaume huyo akikaribia.
"Ni kawaida kwa tembo kulinda watoto wao, watalii wengi hawajui hatari na hawatambui jinsi wanyama hawa wanavyoweza kuwa hatari". Amesema Nel.
Comments