top of page

MTANDAO WA X (TWITTER) KUSITISHA SHUGHULI ZAKE NCHINI BRAZIL

Na VENANCE JOHN


Mtandao wa X zamani kama Twitter umesema unasitisha shughuli zake ndani ya Brazil baada ya kubanwa sana juu ya maudhui inayoyaruhusu. Hii inakuja baada ya Jaji Alexandre de Moraes wa mahakama kuu, kusaini amri ambayo inauagiza mtandao huo kuzifungia baadhi ya akaunti na kutishia kukamatwa kwa mwanasheria wa mtandao huo ikiwa atashindwa kutekeleza amri hiyo.





Mapema mwaka huu, Jaji Alexandre de Moraes alitoa amri ya kuzifuta baadhi ya akaunti zilizotajwa kama wanamgambo wa kidigiti, akimaanisha wanamgambo wanaoendehsa harakati za uasi kwa njia ya mtandao, ambao wamekuwa wakishutumiwa kwa kusambaza taarifa ghushi na za uongo, na jumbe za chuki wakati wa serikali ya mrengo wa kulia ya rais wa zamani wa Brazil Jair Bolsonaro.


Mmiliki wa mtandao huo Bilionea Elon Musk amesema X itafunga shughuli zake mara moja baada ya mfanyakazi wa mtandao huo Rachel Nova Conceicao ambaye ni mwakililishi wa X kwa masuala ya kisheria nchini Brazil kutishiwa kukamatwa.


X (Twitter) ilichapisha nyaraka zilizo sainiwa na Jaji Moraes ambazo zinasema kuwa X itapaswa kulipa pesa ya Brazil reais 20,000, ambayo ni sawa na dola za Marekani 3,653 kiasi sawa na Tsh 9,497,800 (milioni 9.4) kila siku, na kwamba waranti wa kukamatwa kwa mwanasheria wa X nchini humo ungetolewa ikiwa amri hiyo isingetekelezwa. Hii ni nchi ya pili ya bara la Marekani ya Kusini kuibana X baada ya Venezuela kuupiga marufuku mtandado huo kwa miaka 10.

Kommentare


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page