Na VENANCE JOHN
Tangu mwishoni mwa juma hili, wakaazi wa miji kadhaa ya Congo DR hawajaweza tena kuunganishwa na mitandao ya kijamii waipendayo. Uamuzi huo, hata hivyo, unaweza kuwa hauna tija kwa Kinshasa, kwani mzozo huo pia unachukua sura ya vita vya habari.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_344e61f59d3d4f89bf2dc0bc3b7d4caa~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_344e61f59d3d4f89bf2dc0bc3b7d4caa~mv2.jpeg)
Tangu Jumamosi miji ya Goma, Lubumbashi, Kalemie, Bukavu na Kinshasa, watumiaji wote wa mtandao hawana tena ufikiaji wa majukwaa ya X na TikTok. Ingawa kukatwa kwao bado haijathibitishwa rasmi, lakini waangalizi wanakubali kwamba hatua kama hiyo inalenga kukomesha kuenea kwa habari za uwongo kuhusu hali ya mashariki mwa nchi.
Siku ya Jumapili asubuhi, Ange Kasongo alishangaa wakati, alipofungua akaunti yake ya X, ujumbe wa hitilafu ulitokea lakini alipowasha program ya kutumia mtandao binafsi (VPN), kila kitu kilianza kufanya kazi mara moja.
Paulin Ndanda, muuzaji wa simu kwa mkopo katika mji mkuu wa Kivu Kusini, anasema kwake TikTok, aliona habari za uwongo, lakini pia aliweza kutazama video ambazo zilimpunguzia msongo wa mawazo na zilimfanya acheke, zikimruhusu kusahau kidogo kuhusu hali wanayopitia.
Shirika la uchunguzi wa uhalifu wa mtandaoni na utawala wa kidijitali la NetBlocks, lilithibitisha kubaini kwamba ufikiaji wa majukawa hayo umekatishwa. Data iliyokusanywa na shirika hilo inaonyesha zaidi kuwa program ya kupakua program tumishi ya Google Play sasa imezuiwa katika jaribio dhahiri la kuzuia watumiaji kupakua programu za VPN ili kukwepa vikwazo vinavyolenga mitandao hii miwili ya kijamii kutumika nchini humo.
Comments