Mwandishi wa Habari Mwandamizi na mtangazaji wa Kenya, Leonard Mambo Mbotela, amefariki dunia kwa maradhi yaliyokuwa yakimsumbua, tovuti ya Kenyans.co.ke imeripoti. Kifo cha Mbotela (85) kimethibitishwa na mke wa mwanaye anayetambulika kwa jina la Anne Mbotela kuwa mwanahabari huyo aliyehusika kuasisi programu mbalimbali za televisheni nchini Kenya amefariki leo Ijumaa Februari 7, 2025.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_b6ea257b3183426d863131717049f2ed~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_b6ea257b3183426d863131717049f2ed~mv2.jpeg)
Mbotela ambaye alijizolea umaarufu kwa kipindi chake cha "Je, Huu ni Uungwana?" kilichokuwa kikirushwa na Shirika la Utangazaji la Kenya (KBC), alivuta hisia za watu wengi waliokuwa wakimfuatilia.
Kipindi hicho kilianza kuruka mwaka 1966, kikijikita kuhamasisha masuala mbalimbali ikiwemo maadili kimekuwa kikirushwa kupitia Televisheni ya KBC nchini humo. Tangu akiwa shuleni, ndoto yake (Mbotela) katika uandishi wa habari haikupimika, kutokana na ustadi wake wa kusoma magazeti kwa sauti huku akifuatiliwa na wanafunzi wenzake.
Comentarios