Na VENANCE JOHN
Mkurugenzi wa Kinga wa Wizara ya Afya wa Tanzania, Dk Ntuli Kapologwe ameibuka mshindi wa nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa Jumuiya ya Afya ya Nchi za Afrika Mashariki, Kati na Kusini (ECSA – HC) mwa Afrika. Dk Ntuli Kapologwe amewashinda wagombea wengine sita waliokuwa wakiwania nafasi hiyo katika uchaguzi uliohitimishwa leo Jumatano, nchini Malawi.
![](https://static.wixstatic.com/media/57c8da_c9b89857d5984d8db3d2ab414169e00f~mv2.jpeg/v1/fill/w_980,h_980,al_c,q_85,usm_0.66_1.00_0.01,enc_avif,quality_auto/57c8da_c9b89857d5984d8db3d2ab414169e00f~mv2.jpeg)
Dk Kapologwe anachukua nafasi hiyo kutoka kwa Profesa Yoswa Dambisya wa Uganda ambaye amehudumu kwenye nafasi hiyo kwa mihula miwili ndani ya miaka 10. Dk Kapologwe kwa kuzingatia vigezo maalumu vilivyowekwa katika makubaliano ya jumuiya hiyo, ataongoza kwa miaka mitano.
Akizungumza baada ya kuhitimisha uchaguzi huo, Waziri wa Afya wa Tanzania, Jenista Mhagama amesema nafasi hiyo ilipotangazwa mara ya kwanza jumla ya waombaji 47 waliwasilisha wasifu wao na kati yao, saba walichaguliwa kuendelea baada ya mchujo wa awali.
Waziri Mhagama amesema baada ya usaili uliofanywa na kamati ya mkutano wa makatibu wakuu wa nchi wanachama, Dk Kapologwe alipata alama za juu zaidi na kuingia katika hatua ya mwisho pamoja na wagombea wengine wawili kutoka Kenya na Malawi.
Hii ni mara ya pili kwa Tanzania kushika nafasi hii katika kipindi cha miaka 51 cha jumuiya hiyo, kwani kwa mara ya kwanza, Mtanzania Dk Winnie Mpanju alihudumu kama mkurugenzi mkuu kati ya mwaka 1993 na 2000.
Comments