top of page

MTOTO AKAMATWA AKIDAIWA KUMLAWITI MTOTO MWENZAKE..

Kutoka mkoani Njombe Jeshi la Polisi Mkoani humo linamshikilia mtoto wa umri wa miaka (12) kwa tuhuma za kumlawiti mwanafunzi wa darasa la nne (10) katika shule moja iliyopo



Makambako mkoani Njombe.

Hayo yamebainishwa leo Aprili 13, 2024 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Njombe Mahamoud Banga zungumza na waandishi wa habari mkoani hapa.

Amesema tukio hilo lilitokea Aprili 4, 2024 Mtaa wa Jeshini mjini Makambako.

Amesema mwanafunzi huyo alikuwa akilawitiwa kwa ahadi ya kupewa fedha na mtuhumiwa huyo ambaye aliacha shule akiwa darasa la sita.

"Mtuhumiwa huyu anaonekana aliacha shule akiwa darasa la sita lakini amekuwa akimfanyia hivi vitendo kwa muda mrefu kwa ahadi ya kumpatia fedha," amesema Banga.

Amesema kwa muda wote huo mwanafunzi huyo hakusema kwa wazazi lakini tabia yake ilianza kubadilika baada ya kuwa anatokwa na haja kubwa na baada ya mama yake kumuadhibu, ndipo alisema kuwa anafanyiwa vitendo hivyo.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page