top of page

MTOTO WA MIAKA 10 AJIUA KISA KUTANIWA NA MARAFIKI JUU YA MUONEKANO WAKE WA MENO...

Habari za kusikitisha juu ya kisa cha Mtoto wa miaka 10 ambaye ameamua kujitoa uhai baada ya wanafunzi wenzake kuwa na tabia ya kumtania kutokana na muonekano wake wa Meno na



Miwani.

Mtoto huyo aliyetambulika kwa jina la Sammy Teusch, kutoka Greenfield, Indiana, Marekani alifariki kwa kujiua mnamo Mei 5 na, kulingana na familia yake alikuwa akitaniwa sana shuleni.

Ibada ya mazishi ilifanyika Jumatano, Mei 15, Sammy alikuwa darasa la nne katika #GreenfieldIntermediate School na alikuwa akitaniwa na kuonewa na wanafunzi wenzake, kulingana na wazazi wake.

Kwa mujibu wa familia, Sammy alijiua Mei 5 akiwa chumbani kwake.


Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page