top of page

MTOTO WA MWANAMFALME WA NORWAY AKAMATWA KWA TUHUMA ZA UBAKAJI

Na VENANCE JOHN


Polisi wa Norway wamesema kuwa mtoto wa kiume mwenye umri wa miaka 27 ambaye ni mtoto wa Mwana mfalme ambaye anatarajiwa kurithi Ufalme wa Norway amekamatwa kwa tuhuma za ubakaji. Marius Borg Høiby alizaliwa kabla ya mama yake Mette-Marit kuolewa na Mwanamfalme Haakon na kuwa binti wa kifalme mwaka wa 2001.


Alikamatwa kwa kukiuka kanuni za uhalifu zinazohusu kufanya ngono na mtu ambaye hana fahamu au kwa sababu nyinginezo hawezi kupinga kitendo hicho. Polisi wamesema kwamba anatuhumiwa kufanya tendo la ngono bila kujamiiana, kwa mwathiriwa aliyesemekana kuwa hakuweza kupinga kitendo hicho.


Mwathiriwa anayedaiwa ni mwanamke mwenye umri wa miaka 20 ambaye hakumjua Høiby kabla ya kukutana naye siku ya tukio hilo, na hivyo hakuwa na uhusiano na Høiby. Polisi wamesema Høiby alikamatwa Jumatatu usiku, na hata hivyo Høiby amekanusha madai hayo.

Comments


Msasa Media
  • Instagram
  • Facebook
  • X
  • Youtube
  • TikTok

Follow, like, comment, and share

Tel. +255758379300
Mbezi Dar es saalam

bottom of page